Somo la Kwanza: Zef 2:3; 3:12-13
Somo la Pili: 1 Kor 1:26-31
Injili: Matt 5:1-12
Somo la Kwanza: Zef 2:3; 3:12-13
Somo la Pili: 1 Kor 1:26-31
Injili: Matt 5:1-12
Utangulizi
Leo tunasikia hotuba ya Yesu Mlimani. Anatupa maneno ya heri, maneno ya faraja katika maisha yetu. Hizi ndizo nguzo zetu za kutembelea katika maisha ya imani.
Homilia
Heri ya kweli haiko katika nguvu, mali au umaarufu. Bali katika unyenyekevu, unyonge wa moyo na kumtegemea Mungu. Yesu anatuonyesha kuwa thawabu ya maisha ya mwenye kushika hizo heri ni iko mbinguni. Mara nyingi maisha yetu yanavutwa na kufanya kitu kwa ajili ya furaha, umaarufu, nguvu ama fahari ya hapa duniani.
Somo la I: Nabii Sefania anawaeleza watu wake kufuata, haki, unyenyekevu, na kumtegemea Mungu. Mungu anatangaza wazi “nitaacha katikati yako watu wanyonge na maskini, nao watamkimbilia Bwana. Katika somo hili tunaona kuwa Mungu anaunda imani yetu kwake. Mungu hapendezwi na wenye majivuno, bali anaunda jumuiya ya wanyonge wenye imani. Kwa maneno mengine tunapaswa kujivunia uwepo wa Mungu tu katika maisha yetu, ndio msingi wa maisha ya ufalme wa Mungu.
Somo la II: Katika somo la pili Mungu anatuonyesha sifa ama cv anazozitaka katika maisha. Mungu haangalii sifa kama za dunia. Mungu anatenda katika neema. Sio umaarufu wako, sio uwezo wako sio akili yako, sio nguvu zako zinazomfanya Mungu akuchague bali ni Neema yake ndio kigezo chake. Ndio maana Paulo anasema anachagua mambo mapumbavu awaaibishe wenye hekima, tena anachagua vitu dhaifu aviabishe vyenye nguvu.
Injili: Mungu anapanda mlimani kama Musa mpya na kutupatia heri, baraka za Mungu, si kwa maisha ya baadae tu, bali kwa maisha ya sasa pia.
Tumwombe Mungu atujalie kuisimamia Injili na imani yetu hata katikati ya masengenyo, madhulumu, lawama, kusema, kuteswa, kuzushiwa na hata kuonewa. Mungu atujalie kuwa wapole na wanyenyekevu katika kuitetea na kuishi imani yetu.