Usimwogope Yule Ambaye Kwake Hakuna Ufufuko

2025-11-09
Dominika Ya 32 Ya Mwaka, C
Pd. Nicas Mrosso, OFMCap.
📖 Masomo ya Dominika

Somo la Kwanza: 2 Mak 7:1-2, 9-14

Somo la Pili: 2 Thes 2:16-3:5

Injili: Lk 20:27-38

🕊️ Tafakari ya Neno

Utangulizi

Yesu anatuaminifa furaha za uzima wa milele. Furaha hiyo sio kama
ya hapa duniani. Na tusiogope mateso ya hapa duniani kwani hayawezi kuondoa
furaha ya ufufuko. Katika ufufuko hakuna kufa tena. Tumwombe Mungu atujalie
kuamini katika ufufuko wa uzima wa milele.

TAFAKARI
Somo la I: Ndugu saba wanakubali kifo kwa sababu ya ufufuo na uzima wa
milele. Kulikoni kuvunja amri ya Mungu wanakubali kuteseka na kufa.
Hawamwogopi mfalme ambaye kwake hakuna ufufuo. Wanashika kinaganaga
amri za imani ya mababu zao. Ni ukweli kwamba kadir ya imani yao waliamini
kula nyama ya nguruwe ni dhambi. Hivyo walikuwa tayari kufa, kutetea roho
zao kuliko kutenda dhambi.


Somo la II: Sehemu hii ya Barua ya pili kwa Wathesalonike, Paulo
anatuzamisha tena katika uimara wa imani na hasa saburi katika kuungojea ujio
wa pili wa Kristo. Anawaasa Wathesalonike na anatuasa na sisi pia kuwa imara
katika kutenda na kunena mema. Hi ni sawa na kusema kushika amri ama kuishi
Injili.


Injili: Masadukayo waliamini kuwa hakuna kitu kama ufufuo wa wafu. Hii ni
kwa sababu haikuwa wazi katika sheria ya Musa. Na pili kwa sababu
hawakuweza kupata kuelewa itakuwaje. Hii ni kwa sababu ya mazingira pia ya
kihellenistic kuwa, maisha ni hapa duniani tu. Walijiuliza hawa watu huko
inakuwaje, fujo zote za watu wote kuwa sehem moja. Ndio maana wanamuuliza
Yesu mfano huo wa mwanamke aliyeolewa na ndugu saba. Na baada ya kifo
atakuwa wa nani. Pengine itakuwa vita huko.
Yesu aliwapa Jibu linalojitosheleza kuhusu: roho zetu, maisha yetu na maisha
ya baadae yalivyo. Ndio mambo msingi tunayoweza kujifunza leo.

mwili tu. Ukweli ni kwamba tuna Roho. Tuna kitu zaidi ya mwili wetu.
Ndio maana unaweza kukata sehemu ya mwili wako na bado ukabaki
kuwa wewe. Sisi ni zaidi ya kazi zetu, wake zetu, waume zetu, akaunti
zetu, madaraka yetu, hisia zetu n.k.

Hivyo ndugu zangu wapendwa tunaalikwa leo kumwomba Mungu atege
sikio lake juu ya sala yetu ya kuutafuta uzima wa milele kwa kuyapokea maisha
yetu ya hapa dunian kama zawadi kwa Mungu. Na daima tusikubali
malimwengu yatukumbe na kuvunja amri na maagizo ya Mungu.