Somo la Kwanza: Mdo 12:1-11; 2
Somo la Pili: Tim 4:6-8, 17-18
Injili: Mt 16:13-19
Somo la Kwanza: Mdo 12:1-11; 2
Somo la Pili: Tim 4:6-8, 17-18
Injili: Mt 16:13-19
Watakatifu Petro na Paulo ni nguzo mbili za kanisa waliojitoa kwa dhati kueneza kazi Kristo baada ya ufufuko. Ndio waliosia mbegu ya ukristo katika kanisa la mwanzo. Walifuata Njia ya Uzima, waliiungama ukweli, na wakaufia ukweli.
Mtakatifu Petro ni mfano wa uongozi kiimani na mwamwinifu kwa wito wake wa kulichinga kanisa.
Mtakatifu Paulo ni mfano wa ujasiri wa kutangaza Injili, hata kwa gharama ya Maisha.
Watu wanaojitolea kuongoza na kutumikia bila kujitafutia faida binafsi. Bila kuogopa mateso. Wanaotenda kwa imani kubwa.
Kwa pamoja sasa Petro na Paulo, kanisa la mwanzo lilisimikwa imara na likaenea pande zote za dunia. Hakuna kinachoweza semwa kwa kuanzishwa kwa kanisa la Kristo, baada ya Kristo, pasipo miamba hii miwili. Damu yao iliyomwagika inasema zaidi, na sisi tuliokusanyika hapa ni matunda ya Imani yao na ushuhuda wao kwa Kristo.
Tunaposherekea ushindi wao, tunaalikwa kuiga na kupenda Imani yao, maisha yao, majaribu yao, mateso yao, mafundisho yao, na kuwa miamba ya kanisa ya wakati wetu kwa kuusimamia ukweli na kuufundisha.